Jua Cali alikua anastay Calif

Akahama akaenda kustay Hurlinghum, ndume zikasema ooooh, ati Jua Cali sio mreal, ati angebaki mtaa ju uko ndo amegrow up

Angebaki, the same same ndume, zingesema ye ni ngati, ati ako na kamawe, and bado anastay mtaani

Wanyama ako 22 FIFA age, ndume zinazua ati amecheat miaka

Wanyama angesema age ya ukweli, the same ndume zingemwita mbleina ati ye ni fala hajui izi ujanja

Pastor akiambia watu ati waache kufanya dhambi, watu wanampasha ati ooh, ye sio perfect, ati pia ye huangalia denge za wife za wenyewe, ati ooh, sku izi anaomba muhothi sana

Pastor akichorea kushow watu kuhusu sin, inakua ooh, ati ye ni pastor imbo, ati awez zusha ju ya vile anakula sadaka, ati oooh, ati sijui uyu pastor pia hado works yake

Buda akichapa wife, wanasema uyo mjamaa ni Neanderthal, ati heri matha yake angezaa thermos awekange chai, ama quail zimzaliange mayai, ati ohh, kama anajua vita sana, aende aka act na Liam Neeson.

Aspo chapa wife, mara ye ni mnyonge, amekaliwa na wife, ati ye ni mtu ivi ivi, ati ye pia anajifanya mlami na hana pesa

Ukinunua izi T.V zimeenda diet, na pia uweke DSTV, ndume zinsema ati ooohh, ati we ni fala, ati oooh, ati unajifanya Chris Kirubi, na ata fridge yako ni ya kuweka nyanya na mayai pekee, ati ungeweka startimes, ama ununue kale kamashini

Ukibaki na T.V iko na tumbo kaa ya makarao wa traffic, ama ubuy Startimes inakuwa oooh, we ni ngati, ati we unadhani workers wa DSTV hukula mawe, ati ooh, we pia unakazia do, na si ati umejenga nyumba Syokimau

Ukipeleka watoto private, inakua oooh, ati we ni fala, ati waspotokea kwa gazeti hawatenda national, ati ooh, ati hamkuli nyama ndio watoto wasome, ati oooh, masomo sio suruali, mara ooh, ati private zinakula tu pesa

Ukipeleka watoto kanjo, inakua mara we ndio unachangia illiteracy Kenya, ati oooh, ati we ndo unaongeza Sossion kazi, ati we hupendi maendeleo, ati unatesa mtoto

Ukipata mamaa ameiva, inakua oooh, we ni materialistic, ati we humpendi for who she is, ati oooh, ati atakuwacha Ian Mugoya akitoa shati

Ukipata mamaa hajaiva, inakua ati unachoma, inakua oooh, ati we pia huna taste, ati we hujiamini, ati we ni gold-digger

Alfred Mutua akipiga works, inakua ooooh, ye ni Illuminati, ati ako na kiere ere, ati anatafta fame, ati oooh, ati oooooh, ati ata iyo kiwanja ilipaka watu matope, ati CDF ichunguzwe, ati izo gari makarao watakua wanajipiga selfie badala ya kuchase mabandi, ati lazma anakula pesa mingi kama anapea wananchi izo vitu zote

Governor wako aspopiga works, unaanza kusema oooh, ata i wish singevote six piece, ati oooh, uyu governor tutamuimpeach, ati oooh, ati ata ii constitution Kibaki na Raila walitucheat, ati oooh, mara oooh, mara ata 2017 hautavote

Ukiandika update kali, mara umeicopy, mara ata we huandika update moja kali per year

Usipoa toa update kali, ati ooh, we si mcreative, ati we uko chini, ati we unafaa uende brain transplant

WATU HAWATAWAI TOSHEKA

ISHI MAISHA YAKO NA UJIBAMBE, AS LONG AS YOU ARE HAPPY, AND GOD IS TOO

WANAEZA KUPELEKA KWA KIMAIYO

weeki poa

Categories: Opinion

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: